FAHAMU KUHUSU FILAMU YA MAISHA YA 2PAC SHAKUR HAPA





Mtayarishaji wa filamu ya maisha ya marehemu 2 Pac Amesema filamu hii inaanza kufanyiwa shooting katikati ya mwaka 2014. Morgan Creek, Emmett/Furla/Oasis Films na Randall Emmett ambaye ametengeneza End Of Watch na 2 Guns wametangaza kuanza shooting ya filamu hio wiki iliyopita.

Fahamu kuwa filamu hii ilitakiwa kuanza shooting mwaka 2011 ila Morgan Creek na mama wa Tupac, Afeni Shakur walipishana mawazo kuhusu haki na faida za filamu hio.

Filamu itatayarishwa na James G. Robinson, David Robinson, LT Hutton, Randall Emmett na George Furtla. Itafanyiwa shooting mjini Atlanta na itazungumzia maisha ya Tupac na maisha yake ya muziki.

Fahamu Tupac alipigwa risasi mjini Las Vegas, Nevada, ilikuwa September 7, 1996 na kufariki baada ya siku sita.
Previous Post Next Post