CHINI YAPUNGUZA UKALI WA SHERIA YAKE YA KUZAA MTOTO 1 SASA NI RUHUSA KUONGEZA MWINGINE WA PILI TU..!

Serikali ya China jana imesema inatarajia kulegeza vikwazo vya uzazi wa mpango nchi nzima na kuziruhusu familia kuwa na watoto wawili. Hatua hiyo inaoondoa sheria ya kuzaa mtoto iliyodumu kwa miongo mitatu.

Wanandoa wenye mtoto mmoja sasa wana uwezo wa kuongeza mtoto wa pili. Mpango wa kulegeza sera hiyo ulianza kuangaliwa miaka mitano iliyopita baada ya maafisa kuhofia kuwa sheria hiyo inaweza kuzuia ukuaji wa uchumi na kuchangia kuongezeka kwa wazee ambao serikali haina mpango wa kuwasaidia.


Miaka ya 1980s, serikali iliziruhusu familia za kijijini kuzaa mtoto mmoja wa kike na mmoja wa kiume. Sera hiyo mpya itawaathiri wanawake milioni 30 wenye umri wa kuzaa kwenye nchi hiyo yenye watu bilioni 1.4.

Kwa sheria ya sasa, wanandoa wa mjini wanaruhusiwa kuzaa mtoto wa pili iwapo wazazi wote hawana wadogo zao na wazazi wa vijijini wanaruhusiwa kuongeza mtoto iwapo mtoto wao wa kwanza ni msichana. Wanandoa wowote wanaokiuka sheria hiyo hupigwa faini kubwa. Tangu mwaka 1980 serikali ya China imezuia kuzaliwa watoto milioni 400.

Previous Post Next Post