SHEREHE ZA SIKU YA UMOJA WA MATAIFA ZILIVYOFANA ARUSHA


Maaskari wa ICTR wakikamilisha gwaride la kupandisha bendera.

Wanafunzi wakisikiliza mhadhara kwenye ukumbi wa Simba Hall wa AICC.
Sherehe za siku ya Umoja wa Mataifa zimefana sana leo hapa Arusha baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Umoja wa Mataifa ya Rwanda (ICTR) kuwakaribisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari karibu 1000 kutoka shule za mjini Arusha na vitongoji vyake kwenye maadhimisho rasmi. Maadhimisho hayo yalijumuisha upandishwaji wa bendera za Umoja wa Mataifa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; maonyesho ya kazi za mahakama; filamu; na mhadhara kuhusu kazi hizohizo. Sherehe hizo vivile zilihudhuriwa na mamia ya viongozi wa mashirika ya kimataifa yaliyopo Arusha; viongozi wa serikali na mashirika mbalimbali pamoja na viongozi na majaji wa ICTR.

Previous Post Next Post