Muigizaji wa filamu nchini Wema Sepetu amefiwa na baba yake mzazi, Balozi Abraham Sepetu aliyekuwa akiugua kwa muda mrefu maradhi ya kisukari na kiharusi. Alikuwa amelazwa kwenye hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam.
Picha ya Mama yake Wema, marehemu baba yake na dada zake
Kupitia Istagram, Wema aliandika “I love you daddy Sepetu wangu… Dah.”
Kwa mujibu wa mtandao ya Bongocelebrity, mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu maeneo ya Sinza-Mori jijini Dar es Salam.
Balozi Sepetu aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje mnamo miaka ya 1970 wakati wa utawala wa awamu ya kwanza chini ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Vilevile, aliwahi kuwa balozi nchini Urusi tangu mwaka 1982 wakati wa utawala huohuo wa Nyerere. Hadi anafariki, Mzee Sepetu alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Uwekezaji wa Vitega Uchumi Zanzibar.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.

Tags:
Wema Sepetu