GWIJI wa soka duniani, Diego Maradona |
Gwiji na Mkongwe wa soka duniani, Diego Maradona amesema kwamba Mario Balotelli ni mwanasoka nambari nne kwa ubora hivi sasa duniani baada ya Messi, Ronaldo na Neymar.Katika kipindi cha maswali na majibu mjini Milan, gwiji huyo wa Argentina alielezea mapenzi yake kwa nyota huo wa zamani wa Manchester City na kwamba walianza kufahamiana vyema na mshambuliaji huyo wa Italia alipomtumia picha anavuta cigar ya Cuba.
Namba 10 huyo wa zamani, mmoja wa wanasoka bora kabisa kuwahi kutokea duniani alisema: "Mawasiliano yangu ya kwanza na Mario ni pale aliponitumia picha yake anavuta Cuban. Naipenda! Nilicheza,".
Maradona pia anataka kukutana na Balotelli ili ampe ushauri nasaha mshambuliaji huyo wa AC Milan."[Watu lazima] wamuache na amani. Ningependa kuzungumza na Mario peke yetu, katika chumba chetu, na kumfafanulia uzoefu mbaya wote niliopitia.'
Pamoja na hayo, licha ya kuwa shabiki mkubwa wa Balotelli, Maradona anampa nafasi ya nne mshambuiaji huyo wa Milan katika orodha yake ya wachezaji bora duniani, akimuweka nyuma ya Lionel Messi, Cristiano Ronaldo na Neymar.
Wakati huo huo, nyota huyo wa zamani wa Napoli amesema kwamba anapenda kurudi katika klabu hiyo kama kocha mara kocha wa sasa, Rafa Benitez atakapoondoka.
Akiwa ameshinda mataji mawili ya Serie A na timu hiyo miaka ya 1987 na 1990, Nyota huyo wa Amerika Kusini amesema: "Wakati (Rafa) Benitez atakapoondoka ningependa kuikochi Napoli,".
Pamoja na hayo, mtu mzima huyo mwenye umri wa miaka 52 si rahisi sana kwake kupata nafasi hiyo: "Kuna mabadiliko ya makocha yanafanyika kila sehemu kutoka Hispania hadi Italy hadi England hadi Urusi, lakini watu fulani wananiogopa mimi. Ndiyo maana sikochi,."Maradona aliifundisha Argentina hadi kuifikisha Robo Fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2010 na kisha akaenda Dubai kufundisha klabu ya Al Wasl kwa msimu mmoja.
Tags:
Sports