RICK ROSS AENDELEA KUITANGAZA REEBOK LICHA YA KUIKOSA DILI HIYO

Ingawa Rick Ross  alipoteza  dili ya endorsement na kampuni ya Reebok, bosi wa Maybach Music Rick Ross ameendelea kushow love kwa kuvaa viatu vya kampuni hiyo kitu kilichofanya watu wapate maswali ukizingatia mwanzo ilikuwa ni biashara.


                                       Kipindi Rick Ross ana mkataba na Reebok

Rossey ameonesha kuwa hana kinyongo na Reebok kwa kusema kuwa kampuni hiyo ilishow love kwa kufanya naye kazi hapo mwanzo hivyo haoni shida na yeye kuendelea kushow love kwao sasa hata baada ya dili kubuma.

Kwa hali ya kawaida hua inaaminika kuwa mtu maarufu aliyekuwa na mkataba na kampuni hususani ya ubalozi, inapotokea mkataba umeisha vibaya kama ilivyokuwa kwa Rossey, sio rahisi kumuona mtu huyo akiendelea kuipa promo kampuni hiyo, ndio maana maswali yalikuwa je Rossey na Reebok wamerudi katika biashara?

“Not really, not really. It’s just more based on the natural…. what I just feel like rocking, and that’s Reebok a lot of times,” Hilo ndio jibu la Rosssey aliyeulizwa na muwakilishi wa MTV.

Rapper huyo alipoteza dili hiyo ya endorsement na Reebok (April) kutokana na mashairi yake yenye utata katika wimbo wa Rocko “U.O.E.N.O.
Previous Post Next Post