Oprah asema hawezi kuolewa sababu cheo cha ‘mke’ kina majukumu asiyoweza kuyamudu



Usitegemee kumuona malkia wa talk show duniani Oprah Winfrey katika ‘wedding gown’ sababu amekiri kwa kauli yake mwenyewe kuwa hana mpango wa kuolewa licha ya ushawishi aliopata kutoka kwa rafiki yake wa miaka mingi Tina Turner aliyefunga ndoa hivi karibuni.
Oprah-n-stedman
Oprah akiwa na mpenzi wake Stedman
Mwimbaji Tiner Turner ambaye ni rafiki mkubwa wa Oprah alifunga ndoa mwezi (July) mwaka huu, na Oprah alihudhuria sherehe hiyo. Lakini pamoja na ushauri aliopewa na Tina kuwa naye sasa inabidi aolewe, lakini malkia huyo wa Talk show amesema amefanya maamuzi kuwa kwa upande wake ndoa sio kitu kinachomfaa.
Oprah (59) alipoulizwa na Access Hollywood swali la kama hatawahi kuingia kwenye ndoa katika maisha yake yote alijibu “Ndio nadhani hilo ndio jibu langu la mwisho”.
Oprah na stedman2
Aliongeza kuwa alipokuwa katika sherehe ya ndoa ya Tina alijiuliza tena swala hilo baada ya Tina kumsisitiza kufuata nyayo zake naye aolewe. “Because Tina was like, ‘Oprah, you need to do this. You need to do it.’ I was just thinking, ‘Well, OK, would things really be different?’ And no, I don’t think so.” Alisema Oprah.
Oprah na Sted man in Tanzania
Oprah na Stedman walipotembelea hifadhi ya Serengeti, Tanzania July mwaka huu
Oprah ambaye ana mpenzi wa muda mrefu Stedman Graham aliyekuja naye Tanzania katika ziara binafsi mwezi (July) na kutembelea hifadhi ya Serengeti alisema, kama yeye na mpenzi wake wangeamua kufunga ndoa huenda wasingedumu.
“If you ever interviewed him, he would tell you that had we married, we would not be together today,because he’s a traditional man and this is a very untraditional relationship.”
Oprah aliongeza kuwa hawezi kuwa mke wa mtu kwasababu cheo cha ‘mke’ kimebeba majukumu ambayo hawezi kuyamudu.
“I think it’s acceptable as a relationship, but if I had the title ‘wife,’ I think there would be other expectations for what a wife is and what a wife does. First of all, you’ve got to come home sometimes,”.
Previous Post Next Post