Nahodha wa zamani wa Manchester United, Bryan Robson leo ameanza safari ya kuupanda Mlima mrefu zaidi barani Afrika, Mlima Kilimanjaro. Safari hiyo imepewa jina la Kili Trek.
Bryan Robson Enzi zake Akiwa Uwanjani
Timu nzima ya Kili Trek ikiwa tayari kwa safari
Robson anaupanda mlima huo kwa madhumuni ya kukusanya fedha za misaada.
Yeye, mchezaji mwenzie wa zamani, Kevin Moran na watu wengine 25 wanaupanda mlima huo kwaajili ya kuchangisha fedha za Manchester United Foundation.
Mradi huo hufanya kazi na mashirika kama Unicef, Francis House na The Christie Charity kutoa mafunzo ya mpira kwa watu wenye ulemavu na wanaoishi kwenye mazingira magumu.
Robson pia alikuwa akisumbuliwa na saratani ya koo baada ya kupimwa wakati akiwa meneja wa timu ya taifa Thailand miaka miwili iliyopita.

Tags:
Sports