Mtangazaji mkongwe Julius Nyaisangah afariki dunia kwa ugonjwa wa Kisukari

Mtangazaji mkongwe nchini Julius Nyaisangah maarufu kama Uncle J, amefariki dunia leo Alfajiri kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa Kisukari.

Nyaisangah alikuwa Meneja wa kituo cha radio cha Abood FM pamoja na Abood TV cha mjini Morogoro.

Julius Nyaisangah wa mbele akiwa na aliyekuwa mtangazaji mwenzie wa Radio One, Charles Hilary
Kaimu Meneja wa Abood FM, Abeid Dogoli ambaye pia ni Afisa Masoko wa kituo hicho, amesema marehemu Nyaisangah ameacha mke na watoto watatu.

“Kaenda hospitali jana mchana saa nane na amefariki leo Alfajiri lakini kabla ya hapo alikuwa akienda hospitali kupata matibabu na kuweza kurudi,” amesema Dogoli. “Mipango ya mazishi tunasubiri ndugu walioko Dar es Salaam, walioko Tarime ili wakae kama familia wapange msiba utakuwa wapi.”

Pichani ni Watangazaji wa zamani wa Radio One, akiwemo Nyaisangah


Akimuongelea, Nyaisangah aliyewahi pia kuwa mtangazaji wa Radio One, Dogoli amesema Nyaisangah hakuwa tu meneja wa kituo hicho cha radio, bali alikuwa kama mwalimu wa watangazaji na pengo lake haliwezi kuzibika.

“Alikuwa na mtu wa msaada mkubwa kama unavyomfahamu ni mtu unique, ana vitu ambavyo wengine hawana na aliweza kuwabadilisha wafanyakazi wa Abood Media na wakafika sasa kuwa katika hali ya ubora. Kifo chake kimetuhuzunisha sana, kila mtu ameguswa na pengo lake litachukua muda kuweza kupata mtu kuliziba. Kupata mtu wa aina yake itachukua muda.”

Mungu ailize roho yake mahala pema poponi.
Previous Post Next Post

Popular Items