Kampuni ya kutengeza madawa ya GlaxoSmithKline inataka kuruhusiwa kisheria kuidhinisha chanjo ya kwanza ya Malalaria ikisema kuwa imeweza kupunguza vifo vya Malaria miongoni mwa watoto barani Afrika.
Wataalamu wanasema kuwa wana matumaini kuhusu mafanikio ya chanjo hiyo ya kwanza ya Malaria duniani baada ya kufanyiwa majaribio.
Malaria ni ugonjwa unaosababishwa na Mbu na ambao huwaua maelfu ya watu duniani kila mwaka.
Wanasayansi wanasema kuwa chanjo inayofaa ndio njia ya pekee kumaliza ugonjwa wa Malaria.(P.T)
Chanjo hiyo inayojulikana kama RTS,S iligunduliwa kuwa iliweza kupunguza idadi ya vifo vya Malaria miongoni mwa watoto wadogo wakati wa majiribio na pia iliweza kupunguza vifo miongoni mwa watoto wachanga kwa 25% .
Kampuni ya GlaxoSmithKline (GSK) inatengeza chanjo hiyo kwa usaidizi wa wakfu wa Bill na Melinda Gates.
Majaribio ya chanjo yenyewe yalifanyiwa barani Afrika ambako iliwahusisha watoto 15,500 kutoka nchi saba.
Matokeo yaliwasilishwa kwenye mkutano wa matibabu uliofanyika mjini Durban, Afrika Kusini.
Kampuni ya GlaxoSmithKline sasa inataka kisheria iweze kuruhusiwa kuanza kuuza chanjo hiyo ambayo imekuwa ikitengezwa kwa miongo mitatu.
Kwa mujibu wa kampuini hiyo, inataka shirika la afya duniani kuweza kuidhinisha matumizi ya RTS,S angalau kuanzia mwaka 2015 ikiwa wadhibiti wa madawa EMA wanaweza kuwapa leseni ya kuanza kuuza chanjo hiyo.
Kulingana na utafiti uliofanyiwa watoto waliopewa chanjo hiyo, ulionyesha kuwa miezi 18 baada ya kupewa chanjo watoto waliona miezi mitano hadi 17 waliweza kukingwa dhidi ya ugonjwa huo kwa 46% .Lakini watoto waliokuwa kati ya wiki 12 wakati huo waliweza kukingwa tu kwa asilimia 27.
Msemaji wa kampuni ya GSK, aliambia shirika la habari la AFP kuwa kampuni itawasilisha ombi lake chini ya mkakati wa kuziwezesha nchi maskini kuweza kupata dawa.
Tags:
Health