KOMBE LA DUNIA 2014: UJENZI WA MOJA YA VIWANJA WAPIGWA STOP NA MAHAKAMA



brasil 2bf83
Kazi ya ujenzi katika Uwanja utakaochezewa mechi za kombe la dunia la soka mwaka 2014 nchini Brazil zimesimamishwa baada ya jaji wa mahakama kusema kuna wasiwasi kuhusu usalama. (HM)
Uwanja huo wa Arena da Baixada katika jiji la Curitiba ulipangiwa kuchezwa mechi nne za kombe la dunia. Ukarabati wa uwanja huo ulikwishacheleweshwa kwa kipindi kadhaa.
Aliamrisha ukaguzi mpya ufanywe kabla ya kuanza tena shughuli za ujenzi. Akiongeza kusema kumegunduliwa kasoro nyingi katika ujenzi huo.Jaji Lorena Colnago alisema maisha ya wafanyikazi yanahatarishwa kutokana na hali ya kuzorota kwa ujenzi huo. Akiongeza kusema kuna hatari ya kuzikwa,kukanyagwa na magari na hata kudondoka kutoka kuta za juu za uwanja huo.
Taarifa hizo zinakuja wiki moja tu baada ya uchunguzi kufichua kwamba wafanyikazi walioajiriwa katika ujenzi wa mradi mwingine wa kombe la dunia walikabiliwa na hali ya kitumwa.
Wachunguzi hao walisema pia kwamba zaidi ya wafanyikazi 100 walioajiriwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sao Paulo wanaishi katika hali duni karibu na uwanja huo.
Mnamo mwezi wa Agosti, waziri wa michezo Aldo Rebelo alisema ana wasiwasi jinsi ujenzi ulivyochelewa katika viwanja vitano vya michuano ya kombe la dunia mwakani.
Baada ya ziara yake nchini Brazil, katibu mkuu wa FIFA Jerome Valcke,alisema viwanja vyote lazima viwe tayari ifikapo mwezi Desemba na kuonya hatavumilia tena kuchelewesha ujenzi na hakuna 'mpango mbadala'.
Michuano ya kombe la dunia imepangwa katika viwanja 12 nchini kote Brazil. 
Previous Post Next Post