KABURI LA MTOTO SHAABAN MAULID ALIYEFARIKI KISHA KUONEKANA AKIWA HAI ZAIDI YA MIAKA MIWILI ILIYOPITA LAFUKULIWA KWA AJILI YA UCHUNGUZI





Kazi ya Kuchimbua Kaburi imeanza

Uchimbuaji unaendelea na hapa mifupa inaanza kuonekana

Wahusika wa kuchimba Kaburi hilo wanachukua mifupa kwa ajili ya kwenda kwenye uchunguzi

Askari polisi wakiimarisha usalama katika eneo la tukio

Askari Polisi wakiwa wanaimarisha ulinzi wakati wa zoezi la kufukua kaburi
kwa picha zaidi na maelezo bofya soma zaidi

Mabakaki ya mifupa kama yalivyokutwa ndani ya kaburi

Sehemu ya mamia ya watu waliofika kushuhudia tukio hilo

Wananchi wakiwa wamelizunguka gari la polisi wakitaka kujua kilichofukuliwa




Na Denice Stephano,Geita yetu Blog

SIKU chache baada kulipotiwa tukio la mtoto Shaban Maulid (15) anayedaiwa kufariki miaka miwili iliyopita na kuonekana tena akiwa hai, hivi karibuni,kaburi lake anakodaiwa kuzikwa sasa lafukuliwa kwa ajili ya uchunguzi wa kitaalam wa DNA

Tukio la kufukua kaburi hilo lilifanyika Jana 03.10.213 majira saa 08:30 asubuhi na kusababisha shughuli za kawaida katika mji wa Geita na mitaa yake kusimama kwa muda kwa ajili ya wakazi wa maeneo hayo kwenda kushuhudia tukio hilo lililostaajabisha wengi.

Ilipofika majira ya saa moja na nusu asubuhi watu walianza kumiminika nyumbani kwa baba wa mtoto aliyefariki kisha kuonekana na ilipofika majira ya saa mbili maofisa wa jeshi la polisi Mkoani hapa wakiambatana na mtaalamu kutoka ofisi ya mkemia mkuu kanda ya ziwa waliwasili eneo hilo.

Aidha zoezi hilo lilifanyika kwa amani baada ya askari polisi waliovalia sare na makachero kuimarisha ulinzi eneo hilo ambapo mamia ya wakazi wa Geita mjini na wale wa maeneo ya jirani kufurika eneo hilo kushuhudia tukio zima.

Akizungumza mara baada ya kufukua mabaki hayo mkemia huyo kutoka ofisi ya Kanda Lucas Ndunguru alisema wamechukua mifupa miwili mirefu kutoka kwenye miguu yote miwili kwa ajili ya kwenda kupima ili kupata ukweli halisi .

Mtaalamu huyo alisema lengo ni kutaka kujua mtoto aliyepatika kama ndiye mtoto wao halisi pamoja na kujua kilichokuwa ndani ya kaburi hilo,ambapo alisema tayari wazazi wote wamechukuliwa vipimo vya DNA kwa ajili ya kupate ukweli halisi huku akisema wanatarajia baada ya wiki mbili watakuwa wamepata majibu .

"tunakwenda kuchunguza sasa,tayari wazazi wote tumeshachukua vipimo vyao na vile vya mtoto,hatua inayofuata ni kuchunguza na hii mifupa tuliyoichukua kwa ajili ya kulinganisha na baada ya hapo ukweli utapatikana" alisema Lucas

Hata hivyo wakati wakiendelea kufukua kaburi hilo walipofika urefu wa futi moja na nusu walikutana na chungu ambacho ndani yake kulikuwa na mifupa ilisadikiwa kuwa ni ya kuku na kuleta mshangao mkubwa kwa watu .

Mtoto huyo Maulidi Shaban alionekana amefariki ndani ya kisima cha maji Tarehe 01.01.2011 baada kwenda kuchunga Mbuzi kisha kushindwa kurudi nyumbani na baadaye kuonekana baada ya siku tatu akiwa amefia kwenye kisima.

Septemba 30 mwaka huu.mtoto huyo alikutana ana kwa ana na mama yake mzazi Aziza Ramadhan wakati maeneo ya maeneo ya mtaa Mwembeni akitambuliwa kwa kila kitu na wazazi wake hata majirani na walimu wa mtoto huyo wote wakisema ni yeye bila kutia shaka.

Mtoto huyo aliyekuwa akisoma darasa la tano mwaka huo kwa sasa hajaweza kuongea vizuri ambapo kwa mujibu wa daktari wa hospitali ya wilaya Dr.Adamu Sijaona alisema mtoto huyo ataendelea kuwepo hospitalini hapo kwa uchunguzi zaidi wa kiafya ambapo alisema anaendelea vizuri.

Ofisi ya Polisi Mkoani Geita ambayo inafuatilia tukio hili kwa karibu hapa imeendelea kuwaomba wananchi kuendelea kusubiri majibu ya Mkemia mkuu ambapo wananchi hao walitaka kupata majibu siku ya Jana ya kufukua kaburi hilo.


Previous Post Next Post

Popular Items