Huyu Ndiye Aliyeimba Wimbo wa ‘Something About You’ Uliodahniwa ni wa P Square ,Ajitokeza na Kudai Wimbo Huo Ulitoka (2009)


Baada ya kundi la P-Square kutoka Nigeria kukanusha juu ya wimbo ‘Something About You’ uliosambaa kwenye ,mitandao hivi karibuni na kudhaniwa kuwa ni wao, mmiliki wa wimbo huo amejitokeza, anaitwa M-Kaze.



Kwa mujibu wa mtandao wa 360nobs M-Kaze amesema kuwa jina halisi la wimbo wake ni ‘You be the one’ na sio ‘Something About You’ na aliutoa mwaka 2009 kutoka katika album yake iitwayo Psycho.


P-Square

Wiki iliyopita member wa kundi hilo linalotarajiwa kutua bongo mwezi ujao, Peter Okoye alitoa taarifa kwa mashabiki wa P-Square kuwa kundi lao halijatoa wimbo wowote mpya baada ya club banger yao ‘Personally’, ’Peeps pls we haven’t released any other single after PERSONALLY. Thanks’. Aliandika Peter.

Huu ndio wimbo wa M-Kaze uliodhaniwa kuwa wa P-Square



Previous Post Next Post

Popular Items