Fainali za Epiq BSS zazidi Kuyoyoma zaelekea ukingoni mshindi kuondoka na shilingi 50 milioni




Jaji Mkuu wa Shindano hilo Ritha Paulsen akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kinyang’anyiro cha Mwisho cha shindano hilo la Epiq BSS ambapo mshindi atapata shilingi milioni 50 pesa taslimu.
 Ofisa Mtaalam wa huduma za Ziada Cecil Mhina akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu shindano la awamu ya Mwisho Epiq BSS, Kati kati ni Jaji Mkuu wa Shindano hilo Ritha Paulsen na kushoto Ofisa Zantel Haji Yusufu Ramadhan.
 Washiriki mbalimbali wa shindano hilo wakiwa katika picha ya pamoja.
Na Jr Botea #teambongo61
Shindano la Kuimba la Epiq BSS limeingia hatua za Mwisho wiki hii huku likiwa limebakiza washiriki kumi na mbili kuelekea kumpata mshindi wa shilingi milioni hamsini pamoja na mkataba wa kurekodi.
Washiriki waliochaguliwa kwa usaili wa simu, nao waliungana na wenzao waliongia kumi bora wiki hii na kuonyesha uwezo mkubwa, hali inayoashiria kutakuwa na kazi kubwa kumchagua mshindi.
Washiriki waliobaki mpaka sasa na namba zao za ushiriki ni Amina Chibaba (03), Elizabeth Mwakijambile (08), Emmanuel Msuya (21), First Godfrey (11), Francis Flavian (09), Furaha Charles (14), Furaha Mkwama (06), Joshua Kahoza (02), Maina Thadei (5), Mandela Nicholas (10), Melisa John (22) na Raymond John (23).
Akizungumzia hatua ambayo shindano limefikia, Jaji Mkuu wa Shindano hilo, Ritha Paulsen, aliwataka wananchi watumie vema nafasi ya kupiga kura kuchagua washiriki wenye vipaji vikubwa.
“Hatua hii muhimu sana, hasa kwa kuwa inarudisha shindano kwa wananchi ili waweze kumchagua mshindi wao, hivyo nawaomba wawapigie kura kwa wingi,’ amesema Ritha.
Amesema ubora wa washiriki wa mwaka huu, Ritha amesema wamepata washiriki bora zaidi, na pia mafunzo wanayoyapata ndani ya jumba la Epiq BSS ni makubwa hivyo mashabiki watarajie mchuano mkubwa zaidi katika kuwania milioni hamsini.
Kwa upande wake, Afisa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan, amewataka wananchi wawapigie kura washiriki wanaoamini ni wazuri na watafanya vizuri kwenye soko.
“Maana ya kufungua laini za watu kupiga kura maapema ni kuwapa nafasi ya kuchagua mshindi wanayempenda,” amesema Khan.
Kampuni ya Zantel pia imerahisisha namana ya kupiga kura kwa kutoa namba maamlumu ya kupiga simu namba 0901551000, na kwa njia ya ujumbe mfupi mashabiki wa Epiq BSS wataweza kuwapigia washiriki wanaowapenda kwa kuandika neon KURA, halafu waache nafasi, namba ya mshiriki halfu watume kwenda 15530.
Previous Post Next Post

Popular Items