Bill Gates ashinikizwa kuachia ngazi ya uenyekiti wa Microsoft



Wawekezaji wakubwa watatu wa kampuni ya Microsoft ya Marekani wamemshinikiza mwenyekiti wa kampuni hiyo Bill Gates aachie ngazi ya uenyekiti baada ya kukalia kiti hicho kwa miaka 40 toka ilipoanzishwa.
Kwa mujibu wa Skynews ripoti zinasema kuwa wawekezaji hao wanadai kuwa uwepo wa Mr Gates katika bodi ya wakurugenzi inazuia mabadiliko ya mbinu mpya za maendeleo ya kampuni hiyo na kuweka ugumu kwa Chief executive wa sasa kufanya mabadiliko makubwa.
Taarifa hii imekuja siku chache toka CEO wa Microsoft Steve Ballmer kutangaza kujiuzulu ndani ya mwaka mmoja kufuatia shinikizo kutoka kwa waungaji mkono, wakati kampuni inajipanga upya na mapambano ya ushindani mkubwa katika sekta ya teknolojia.
Hata hivyo Microsoft bado ni moja kati ya makampuni ya teknolojia yenye thamani duniani, na hisa zake zimeendelea kubaki na thamani kwa takribani miaka 10 kutokana na nguvu ya Ballmer ya kupambana na Apple na Google.
Bill Gates alikuwa Chief Executive Officer wa Microsoft mpaka mwaka 2000 alipomuachia Ballmer nafasi hiyo na yeye kubaki kuwa mwenyekiti.
SOURCE: SKY NEWS 
Previous Post Next Post