Kaa Tayari kuona vituko na sherehe za uswazi jinsi zilivyo kwenye video mpya ya Shaa, Sugua Gaga. Shaa ambaye kwa sasa yupo chini ya usimamizi wa kampuni ya Mkubwa na Wanae ya Said Fela, ameshoot video ya wimbo huo maeneo ya Magomeni jijini Dar es Salaam,wakati Muongozaji wa video hiyo ni Adam Juma.