Adai Muziki Hauna Maana na Faida Katika Maisha Yake



Mkali wa Staili za Kuflow na Rapper wa Chamber Squad, Noorah aka Babastlyez amesema hana hamu kubwa tena ya kufanya muziki kwakuwa haumnufaishi kwa chochote.




Akizungumza na DJ HAAZU katika kipindi cha Dundo cha MJ RADIO Arusha, Noorah ambaye hivi karibuni alifunga pingu za maisha, alisema muziki hauna faida kwake na kwa sasa anaufanya kama starehe tu.

“Maisha ni malengo, kitu hata kama unaweza vipi, hata kama watu wanakupenda vipi kwenye hicho kitu, kama hakina manufaa mazuri kwako, hakina maana kwako,” alisema Noorah.

“Mimi muziki kama naufanya, naufanya kwa starehe zangu tu, haya mambo ya kutoa single, ifanye hivi, biashara hiyo sasa hivi haipo kwangu.”

Noorah aliongeza kuwa muziki wa Tanzania una siasa nyingi kiasi ambacho hata wale wanaonekana wamefanikiwa hawana lolote.

Msikilize hapa.


Previous Post Next Post