Viongozi wa dunia wanaokutana katika mji wa St. Pettersburg nchini Urusi kwa kongamano la mataifa ishirini yenye uwezo mkubwa wa kiviwanda G20 wameshindwa kukubaliana kuhusu hatua zinazofaa kuchukuliwa dhidi ya Syria huku msemaji wa serikali ya Urusi akisema kuna mgawanyiko mgkubwa kuhusiana na swala hilo.
Duru zinaarifu kwamba viongozi wa Uingereza, Ufaransa, Uturuki na Canada wanaunga mkono azimio la rais wa Marekani Barrack Obama kuishambulia Syria kijeshi kutokana na madai ya serikali ya rais bashar al Assad kutumia silaha za kemikali.
Lakini rais wa Urusi, Vladimir Putin, amesema kuwa bado haijabainika ni upande upi ulitumia silaha hizo.
Wakati huo huo Balozi wa Marekani katika Umoja wa mataifa Samantha Power ameikashifu Urusi kwa kuzuia umoja wa mataifa kuichukulia Syria hatua.
Umoja wa mataifa unasema kuwa unahitaji dola bilioni tatu unusu zaidi kukabiliana na tatizo la wakimbizi kutuka Syria hadi mwisho wa mwaka huu.
Afisa mkuu wa shirika la umoja huo kuhusu haki za kibinadamu,Valerie Amos, ameiambia BBC kwamba mataifa wafadhili yanastahili kutathmini upya mchango wao na kuyataka kuwa wakarimu zaidi.
Umoja wa mataifa unakadiria kwamba watu milioni mbili wamekimbia Syria na wengine milioni nne wanaishi maisha ya ukimbizi nchini Mwao.
Valarie Amos anasema masaibu ya Wasyria yana uzito mkubwa kuhusu usalama ana amani ya dunia kutokana na idadi kubwa ya watu wanaokimbia kufuatia shambulizi la silaha za kemikali.
Tags:
Politics