Klabu ya Arsenal jana imekamilisha usajili wa kiungo wa kimataifa wa Ujerumani Mesut Ozil kwa ada ya uhamisho ambayo imevunja rekodi ya usajili ya klabu hiyo.
Arsene Wenger amewatimizia ahadi mashabiki wa klabu hiyo kwamba atasajili mchezaji bora mwenye jina kubwa katika dirisha la usajili ambao lilifunguliwa Julai na kufungwa September 2.
Lakini pamoja na usajili huo wa Ozil, wachambuzi wa mpira duniani wanasema kwamba Ozil ataisadia Arsenal, lakini klabu hiyo bado haijapata ufumbuzi wa matatizo yao makubwa ambapo ni kwenye ulinzi na ushambuliaji kidogo.
Arsenal pamoja na kushika nafasi ya nne kwenye ligi ni timu ambayo ilikuwa miongoni mwa vilabu vilivyokuwa vikiongoza kwa kutengeneza nafasi nyingi za kufunga kupitia viungo wake Aaron Ramsey, Rosicky, Santi Cazorla, Jacky Wilshare na mawinga kama Theo Walcott na Lukas Podolski. Tatizo kubwa la Arsenal katika misimu kadhaa iliyopita limekuwa kwenye nafasi ya kiungo cha kukaba na upande wa ukuta wao nyuma.
Lakini mpaka dirisha la usajili linafungwa timu hiyo haijasajili beki hata mmoja huku wakiwa na mabeki wao wale wale ambao kiukweli wamekuwa wakiiangusha sana timu hii.
Ni sawa wamemsajili Ozil - lakini walikuwa na mahitaji makubwa kwenye nafasi ya kiungo cha ushambuliaji kama ilivyokuwa kwenye nafasi ya ulinzi kwa maana ya mabeki?
Ni namna gani Arsenal wataweza kumtumia vizuri Ozil ambaye ana sifa ya upishi wa mabao - ndani ya timu yao?
Je usajili wa Ozil uliogharimu fedha nyingi kuliko wowote katika Premier League msimu huu ni sahihi kwa mahitaji ya Arsenal?
***************TOA MAONI YAKO TUJADILI*************
***************TOA MAONI YAKO TUJADILI*************
Tags:
Sports