Idadi ya watu waliopoteza maisha kufuatia shambulio la kigaidi kwenye mall ya Westgate ya jijini Nairobi, imefikia watu 69 na wengine 175 wakijeruhiwa.
Mtu na mpenzi wake waliouwa kwa pamoja na wanamgambo hao, walikufa wakiwa wamekumbatiana |
Mwanamke aliyekuwa amejeruhiwa akiomba msaada
Akihutubia Jumapili, Sept 22, kutoka ikulu jijini Nairobi, Rais Kenyatta alisema zaidi ya watu 1,000 wametolewa nje ya mall huyo na shughuli za uokozi zinaendelea.
Inadaiwa kuwa magaidi 10 au 15 wa kundi la Kisomali la Al-Shabab bado wamo ndani na bado kuna watu wengine ndani ya mall hiyo, wakiwa mateka ama wamejificha.
Familia ikiwa imeshikana mikono wakati ikitoka nje ya eneo la hatari
“Wahalifu hao wapo kwenye sehemu moja ndani ya jengo,” Rais Kenyatta alisema. “Kukiwa professionals kwenye eneo hilo, tuna nafasi nzuri ya kuwatuliza magaidi kama tunavyoweza kutazamia.”
Rais huyo aliwashukuru wale waliosaidia shughuli za uokozi na msaada na ameziomba nchi nyingine zisitoe maagizo ya watu kutembelea nchini Kenya. Mpwa wa Kenyatta aliyekuwa na mchumba wake ndani ya mall hiyo ni miongoni mwa watu waliouawa.
Mama na wanae akiwa amejificha kuhofia kuuawa na watu hao makatili
Mfanyakazi wa Red Cross akimbeba mtoto aliyekuwa ndani ya mall hiyo
Mtoto akikimbia kuokoa maisha yake
Mtoto akiwa nje baada ya kutolewa ndani ya mall, pembeni ni mwili wa mtu aliyeuawa
Kuna ripoti kuwa magaidi hao kwa sasa wamejikusanya kwenye supermarket moja. Rais Kenyatta alisema kulikuwa na taarifa zingine kuwa miongoni mwa watu hao wamo wanawake pia. Kundi la Al-Shabab limedai kuwa limewashikilia mateka 36.
Mwanamke akilia kwa woga baada ya kuokolewa na askari
Mwanamke aliyejeruhiwa akitolewa nje kwa kubebwa kwenye toroli la kufanyia shopping
Mwanamke aliyekuwa ameshikiliwa mateka akiwa haamini baada ya kuachiwa
Maafisa wamesema watu hao wamebananishwa na kwamba watu wameshikiliwa mateka kwenye maeneo mbalimbali. Al-Shabaab imeliambia shirika la habari la Uingereza BBC kuwa limefanya shambulio hilo kujibu opereshini za kijeshi za Kenya zinazoendelea nchini Somalia.
Mwanaume aliyejeruhiwa akilia kwa uchungu kutokana na maumivu makali baada ya kupigwa risasi ya mguu
Ofisa wa usalama na wenzake wakielekezana mahali walipo watu hao wenye silaha
Polisi akisaidia kumtoa mtoto aliyekuwa ndani ya mall
Polisi na wanajeshi wakipambana na magaidi hao
Polisi wa Kenya akiwa ameshika tumbo lake baada ya kujeruhiwa huku mwenzake akiendelea kurushiana risasi na magaidi wa Al-Shabaab
Polisi wakiingia ndani ya mall hiyo kupambana na wana mgambo wa Al-Shabaab
Polisi wakipambana na Al-Shabaab
Raia wa Canada Annemarie Desloges, 29, aliuawa kwa risasi na magaidi hao
Wanajeshi walimwagwa kwenda kusaidia kupambana na watekaji wa kundi la kigaidi la Al-Shabaab
Wananchi wa mataifa mbalimbali waliokuwa wakifanya shopping kwenye mall hiyo wakiwambia kuinua mikono yao kuonesha hawana silaha
Wananchi wakikimbia kuokoa maisha yao
Wanawake na watoto wao wakihaha kuokoa maisha yao ndani ya mall hiyo
Wanawake waliojeruhiwa wakisaidiwa
Watu mbalimbali wakijaribu kuokoa maisha yao wakati watu hao wenye silaha wakiwa ndani ya mall
Watu wakimsaidia kumdaka msichana aliyekuwa amejificha ndanii ya mall hiyo
Watu wakisaidiwa kutoka nje ya mall, pembeni ni mwili wa mtu aliyeuawa
Watu waliokuwa ndani ya Westgate wakisaidiwa kutoka nje na askari
Watu waliokuwa wakifanya shopping wakisaidiwa kutoka nje ya mall na askari