Picha: TCRA yaendesha warsha ya siku mbili kwa wamiliki na waendeshaji wa blog Tanzania 'Leo ni Siku ya Mwisho'




Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, TCRA leo imefungua warsha ya siku mbili kwaajili ya wamiliki na waendeshaji wa blogs na website nchini ya namna ya kuziendesha kwa ufanisi na kwa maendeleo ya taifa.


Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma akiwasilisha mada kuhusu hali ilivyo katika sekta ya Mawasiliano nchini

Warsha hiyo inafanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, jijini Dar es Salaam.

Akiongea wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Prof. John Nkoma, alisema mamlaka hiyo imefanya warsha hiyo kwakuwa inapenda kuona blogs na website za Tanzania zinapiga hatua zaidi. Alisema utafiti wa mamlaka hiyo umebaini kuwa siku za mbeleni watu wengi watakuwa wakitumia zaidi simu kupata huduma ya internet na kwamba licha ya Tanzania kuwa na watumiaji zaidi ya milioni 27 wa simu, ni watu milioni 7.5 pekee wanaifikia huduma hiyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti Mtendaji wa Google Africa Joe Muchiru aliyekuwa miongoni mwa watoa mada, alidai kuwa siku zinavyoenda, makampuni madogo na makubwa duniani yameanza kutegemea zaidi kutangaza bidhaa zao mtandaoni kwakuwa yanawafikia watu wengi.


Mwenyekiti Mtendaji wa Google Africa, Joe Muchiru akiwasilisha mada kuhusu uchaguzi wa mtandao bora wa kijamii kufikisha ujumbe na jinsi ilivyo na nguvu


Alisema katika miaka ijayo, makampuni mengi duniani yatakuwa yakilipa pesa nyingi kutangaza mtandaoni kuliko hata ilivyo kwenye TV. Hata hivyo Muchiri alitoa tahadhari kwa blog zenye matangazo mengi juu yanayoishia kumaliza data za mtumiaji wa internet ambaye huogopa kuzifungua.


CEO wa Google Africa, Joe Muchiri na MD wa Tech Walk Liz Wachuka wakifuatilia kwa makini mada iliyokuwa ikiwasilishwa

“Ndio, mteja anakulipa wewe lakini mwisho unajikuta ukipoteza kwasababu wasomaji wataanza kukukimbia,” alisema Joe.

“Hii ndio sababu unakuta Google haiwezi kuweka matangazo kwenye frontpage hata kama kuna watu wako tayari kulipa mabilioni kuwa kwenye frontpage ya Google. Google inasema ‘hatuwezi kutangaza pale’.”


Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy


Mmiliki wa blog ya Michuzijr, Ahmed Michuzi akibadilisha jambo na blogger mwenzie


Mtangazaji wa Passion FM na mwandishi wa vitabu, Adela Kavishe akihudhuria warsha hiyo

Akizungumzia umuhimu wa mitandao ya kijamii hususan Facebook na Twitter, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Tech Walk, Liz Wachuka, alidai kuwa huko ni sehemu kwa makampuni kujitangaza, watu kuwasiliana, kufahamiana na kujifunza lakini inatakiwa kutumiwa vyema na si kwa kuchafuana.


Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Tech Walk, Liz Wachuka akiwasilisha mada kuhusu utumiaji wa mitandao wa kijamii kwa mambo msingi


Jeff Msangi na Jestina George


Jestina George


Joseph Mwaisango wa Mbeya Yetu blog


Othman Michuzi wa Mtaa kwa Mtaa blog na Mwandishi wa gazeti la Mwanachi, Henry Mdimu


Shamim Mwasha wa 8020 Fashions





















Warsha hiyo inaendelea tena leo.
Previous Post Next Post

Popular Items