Mr Nice aingia kwenye mgogoro mwingine....



Mwanzilishi wa style ya ‘Takeu’ Lucas Mkenda a.k.a Mr Nice ameingia tena kwenye mgogoro na meneja wake mpya wa Candy & Candy baada ya kutokukubaliana baadhi ya mambo aliyokuwa akishauriwa na lebo hiyo.

Akizungumza na MWANANCHI mkurugenzi wa Kampuni ya Candy & Candy Records, Joe Kariuki alisema kampuni yake na Mr Nice anayependwa nchini Kenya walitofautiana katika baadhi ya mambo hasa ubora wa kazi.

“Mr Nice ni msanii anayependwa sana hasa Mombasa, lakini wiki chache zilizopita tulikuwa na mabishano kidogo hii ilitokana na mtazamo tofauti hasa ni kutokana na wimbo wake mpya wa ‘Akina Mama’ binafsi ule wimbo sikuupenda na nilimshauri kwamba ni vyema tungetumia wimbo mwingine, lakini aling’ang’ania”

Aliendelea kusema “Wimbo ule tuliupiga katika vyombo vya habari kwa bahati mbaya haukufanya vizuri lakini nilimtahadharisha mapema.

Kariuki aliongeza “Kampuni inaweza kupata hasara, lakini tumeamua kuendelea na mkataba kwani kwa sasa ameelewa na tunakwenda kama kampuni inavyotaka,” alisema Kariuki kampuni hiyo imeingia mkataba na wasanii wengine kutoka nchini Tanzania wakiwamo Four – D, Top C, Mr Nice na Baby Madaha

Mr Nice hapo awali alikuwa na mkataba na lebo ya GrandPa Records ambayo walishindwana na kuamua kuvunja mkataba na sasa yupo na Candy & Candy Records
Previous Post Next Post