Chege na Temba Wapata Shavu la Shoo Ulaya Ni Miezi Mitatu 'Kuanza wiki Ijayo'




Wasanii wa kitambo wa Kundi la TMK Wanaume Family Chege na Temba wanatarajia kuanza ziara ya miezi 3 barani Ulaya kuanzia wiki ijayo.



Akizungumza na Bongo5 meneja wa kundi hilo Said Fella amesema kesho ndio wanategemea kupata Visa na wiki ijayo (September 25) Chege na Temba wataondoka nchini wakielekea nchini Sweeden ambako watafanya show ya kwanza (October 5).

Temba na Chege watashiriki show za Serengeti Fiesta Musoma siku ya Ijumaa hii na kumalizia Shinyanga siku ya Jumapili zikiwa ndio show zao za mwisho za Fiesta kabla ya kuondoka nchini .

Msanii mwingine wa Bongo Ommy Dimpoz aliondoka nchini Jana kuelekea Marekani ambako atakuwa na show kadhaa kabla hajarejea nchini kushiriki fainali ya Serengeti Fiesta Dar es salaam, huku Diamond Platnumz naye anatajaria kwenda nchini Malaysia wiki ijayo ambako atafanya show (September 20) kufanya show.
Previous Post Next Post

Popular Items