Maseneta wawili mashuhuri wa Marekani wamesema uongozi wa rais Barack Obama unaweka pamoja mpango mahsusi kuunga mkono upinzani nchini Syria na kusaidia kumtimua madarakani rais Bashar al- Assad.
Mrepublican John McCain na Lindsey Graham ambao wanaunga mkono hatua ya kijeshi dhidi ya Syria walikutana na rais Obama White House Jumatatu.
Naye rais wa Russia Vladmir Putin amesema anaunga mkono wazo la kutuma wajumbe mjini Washington kujadiliana na wabunge wa Marekani kutounga mkono hatua ya kijeshi dhidi ya Syria.
Valentine Matviyenko mwenyekiti wa baraza la bunge la Russia alielezea mapendekezo ya kutuma ujumbe wa wabunge nchini Marekani wakati alipokutana na rais Putin Jumatatu.
Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Sergei Naryshkin spika wa bunge la wawakilishi la Duma. Atviyenko alisema anategemea mjadala wenye mafanikio na wabunge wa Marekani kuhusu swala la kuvamia Syria
Tags:
Social