MAN UNITED YASHINDA 4-2 ULAYA, ROONEY AFUNGA MAGOLI 2





Wayne Rooney Akifunga bao (HM)



KOCHA David Moyes ameonyesha nini alihitaji kucheza soka ya wazi, soka adimu Uwanja wa Old Trafford, ambayo matunda yake ni kushinda mabao mengi, 4-2 dhidi ya Bayer Leverkusen ya Ujerumani katika mchezo wa kwanza wa hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa usiku wa kuamkia leo.

Hadi sasa, Moyes wakati wote amekuwa akijaribu kuwatumia pamoja Robin van Persie na Wayne Rooney pale mbele. Sasa wako upande wake na wanamfanyia kazi nzuri.

Van Persie amefunga moja ya mabao ya msimu, Rooney amefunga mawili na lingine Antonio Valencia katika ushindi ho na sasa wanaelekea kwenye mchezo dhidi ya mahasimu wao, Manchester City wakiwa wenye kujiamini.

Faraja kwa Rooney leo ametimiza mabao 200 ya kuifungia United, hivyo kuingia kwenye orodha ya magwiji wa klabu, Bobby Chartlon mabao 249, Dennis Law 237 na Jack Rowley 211.
Katika mechi hiyo iliyochezeshwa na refa Damir Skomina wa Slovenia, Rooney alifunga dakika ya 22 na Bayer wakasawazisha kupitia kwa Rolfes dakika ya 54, kabla ya Van Persie kufunga la pili dakika ya 59, Rooney tena la tatu dakika ya 70 na Valencia dakika ya 79 kabka ya wageni kupata bao la pili dakika ya 88 kupitia kwa Toprak.

Kikosi cha Man Utd kilikuwa: De Gea, Smalling, Ferdinand, Vidic, Evra, Valencia, Carrick, Fellaini/Cleverley dk81, Kagawa/Young dk71, Rooney/Hernandez dk84 na Van Persie.

Bayer Leverkusen: Leno, Donati, Spahic, Toprak, Boenisch, Can, Reinartz, Rolfes, Sam/Kruse dk78, Kiessling/Derdiyok dk78 na Son/Benderdk 64.Uteuzi wa timu wa Moyes unamaanisha Ryan Giggs atasubiri sana kuongeza idadi ya mabao yake.

Mkongwe huyo wa United, akiwa amebakiza miezi miwili kusherehekea kutimiza miaka 40, amefungana kwa na gwiji wa zamani wa Real Madrid, Raul katika kucheza mechi nyingi katika Ligi ya Mabingwa, wote 144).

Na kwa kuwa Giggs hakuwepo hata benchi, kuna uwezaekano ikamchukua muda sana. Giggs na Raul wanafuatiwa na Paolo Maldini (mechi 140), Xavi (mechi 136), Clarence Seedorf (mechi 131), Paul Scholes (mechi 130) na Iker Casillas (mechi 129). 

Credit: binzubeiry
Previous Post Next Post

Popular Items