Msanii wa THT, Linah Sanga amesema hakuna mtu anaweza kumloga katika muziki kama wasanii wengine walivyo na wasiwasi wa kufanyiwa hivyo ama kutembelewa nyota zao.
Linah amesema hayo jana, wakati akielekea kwenye Serengeti Fiesta Mtwara na kushangazwa na baadhi ya wasanii kutangaza kulogwa kila wakati.
“Hakuna mtu anayeweza kuniloga kwakuwa namtumainia Mungu kwa kila jambo ninalolifanya katika maisha yangu, alisema mrembo huyo.
Linah aliongeza kuwa kabla ya kuingia kwenye muziki alikuwa akiiimba nyimbo za gospel wakati huo baba yake alikuwa mchungaji wa kanisa, kitu ambacho kilimpa woga wa kuingia kwenye muziki wa dunia kutokana na baba yake kumzoea akiimba nyimbo za injili.