Kendrick Lamar aahirisha tour Yake ya Afrika Kusini



Kampuni ya Miller Genuine Draft ya Afrika Kusini, leo imetangaza kuwa rapper Kendrick Lamar aliyekuwa anatarajiwa kuwa na ziara nchini Afrika Kusini mwezi November mwaka huu ameahirisha hadi February 2014.


Kendrick amebadilisha ratiba hiyo ili kumpa kampani Kanye West atakayekuwa na ziara ya Marekani itakayoanza mwezi ujao hadi katikati ya December.

Mashabiki waliokuwa wamenunua tiketi kushuhudia show zake watalazimika ama kurudisha tiketi hizo ili warudishiwe hela yao ama kubadilisha tiketi kwaajili ya show ya mwakani.

Ratiba mpya ya ziara ya Kendrick Lamar nchini Afrika Kusini itaanza February 2014 jijini Durban ikifuatiwa Johannesburg na Cape Town
Previous Post Next Post