
Kama tunavyojua chunusi hazitakiwi kusababisha makovu lakini ukitumbuaji au kubadua chunusi kunasababisa makovu kwenye uso au mwili.

Kama unamakovu ya chunusi kuna namna nyingi ya kuweza kuyaondoa makovu hayo lakini treatment zake zinaweza kuwa na maumivu sana au za ghali sana lakini kuna njia za kihalisia za kuweza kuondoa makovu hayo.

1.Paka bleach cream kwenye sehemu zenye makovu ambapo cream hii husaidia kuyangarisha makovu

2.Pia unaweza kutumia kuondoa ngozi ya juu (Exfoliate) kwa kutumia facial body scrub kwa sehemu zile zenye makovu lakini inategemea na sehemu gani ya mwili. Uondoaji huu wa layer ya juu (Exfoliate) unaweza kufanya angalau mara mbili kwa wiki.

3.Tumia product ambazo zina `hydroxy acids` hii acid hutokea kihalisia na hutibu ngozi yako na vile vile ngozi yako itaonekana younger and smoother, na makovu ya chunusi hupotea. Unaweza kupata hydroxy acids tofauti tofauti za skin care products kam vile cleansers, lotion na serums.

4.Pia unaweza kumassage makovu ya chunusi kwa maana massage hushauriwa kwa ajili ya mzunguko wa damu ambapo husaidia hufika katika sehemu zile zenye makovu ambapo tunaambiwa massage pia husaidia sana kuvunja scar tissue.


Tags:
Beauty