Brigitte Alfred awa mshindi wa 3 wa shindano la ‘Beauty With a Purpose’ la Miss World 2013



Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred ameibuka mshindi wa tatu kwenye shindano la ‘Beauty With a Purpose’ la Miss World 2013 ambalo fainali yake ni kesho nchini Indonesia. Shindano hilo ni miongoni mwa mashindano mengine manne yanaoenda sambamba na fainali za Miss World.



Shindano hilo huhusisha shughuli za kusaidia jamii zinazofanywa na warembo hao kwenye nchi zao na kuwa chachu za mabadiliko kwenye jamii hizo. Mradi wa Brigitte ulihusisha kutembelea walemavu wa ngozi mkoani Shinyanga ambao maisha yao huwa yapo hatarini kutokana na mauaji ya imani za kishirikina.




Baada ya kuwa mshindi wa tatu, mrembo huyo aliandika kupitia Instagram: Jumping for joy:) 3rd in beuty with a purpose!Super happyyy right now! #Tanzania.”

Kesho mrembo huyo atapanda jukwaani kwenye fainali za Miss World nchini Indonesia kuipeperusha bendera ya Tanzania.
Previous Post Next Post