Benki ya Uingereza ya Barclays inasema itasitisha biashara na kampuni zinazosafirisha fedha huko Somalia, hapo septemba 30. (HM)
Benki hiyo ina wasi wasi kwamba kampuni hizo za kusafirisha fedha, zinazofahamika zaidi Somalia kama Hawala zinatumiwa kugharimia ugaidi.
Lakini mashirika ya huduma za dharura nchini humo wametoa wito kwa Barclays kuahirisha mpango wake ili kuweza kupatikana mpango mbadala wa kuchukua nafasi ya kampuni hizo ambazo wasomali wengi wanategemea .
Hawala njia ya kusafirisha fedha kwa simu ni moja wapo ya biashara kubwa Somalia inayotumiwa na maelfu na maelfu ya wasomali kupeleka na kupokea fedha kutoka nchi.
Barclays iilitishia kufunga akaunti za makampuni hayo mara mbili hapo awali lakini kubadilisha mpango kutokana na malalamiko makubwa. Umoja wa mataifa unakadiria kwamba Somalia hupokea dola bilioni 1 na nusu kila mwaka kutokana na fedha zinazopelekwa na wasomali wanaoishi n'gambo.
Credit: voaswahili
Tags:
Business