Baada ya Matukio ya Westagte Mall: Kampuni iliyokata bima ya Westgate yakabiliwa na bili ya Kshs bilioni 6.6 kufuatia shambulio la kigaidi



Pressure za mabosi wa kampuni ya bima yenye makao yake jijini London, Uingereza The Lloyd’s market ipo juu baada ya jengo la Westgate ya Nairobi, Kenya iliyokuwa imekata bima kwenye kampuni hiyo kushambiliwa na magaidi Jumamosi iliyopita na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 70.



Zaidi ya maduka 50 yalikuwa ndani ya mall hiyo zikiwemo ofisi za Nakumatt Supermarkets, Barclays Bank, migahawa, maduka ya vidani na nguo, yote yamepata hasara kubwa ambayo haijajulikana bado.

Watu zaidi ya 500 waliokuwa wakifanya kazi humo nao wamebakia bila kazi na tangazo la kuwa ghorofa tatu za jingo hilo zimeanguka linamaanisha kuwa itachukua miezi kibao hadi mambo yarejee kama mwanzo.



Imebainika kuwa Sony Holding Limited, kampuni ya nyumba inayomilikiwa na Alex Tachenberg, ilikata bima kwaajili ya jengo hilo kupitia kampuni ya Lloyd’s ya thamani ya shilingi bilioni 6.6 za Kenya.

Gazeti la The Times la India liliripoti kuwa ujenzi wa jengo hilo uliosimamiwa na nguli wa ujenzi Lakshman Raghavani wa India uligharimu shilingi bilioni 4.2 za Kenya.

Kampuni ya Knight Frank inayothamanisha mali ililiambia gazeti la Business Daily kuwa jengo hilo haliwezi kuuzwa chini ya shilingi bilioni 6.9 za Kenya.

Source: Business Daily
Previous Post Next Post

Popular Items

WAKUU WA USALAMA KUHOJIWA KENYA