Rapper Soulja Boy, 23 wiki iliyopita alijikuta akiteremshwa ndani ya ndege ya shirika la American Airlines baada ya kukataa kuheshimu maelekezo ya mhudumu wa ndege.
Staa huyo Kiss Me Through the phone aliponea chupuchupu kukamatwa na maofisa wa usalama walioitwa ndani ya ndege hiyo kumshusha.
Mtandao wa TMZ umeripoti kuwa staa huyo ambaye jina lake halisi ni DeAndre Cortez Way – alikataa kukaa chini wakati wa maelekezo ya usalama ya ndege licha ya kuombwa mara nyingi.
Staa huyo alikuwa anatokea Miami, Florida, kuelekea kwenye show Brazil.