Mchezaji wa mpira wa kikapu wa ligi ya NBA ya Marekani,Stephen Curry na mwenzake ambaye ni Mtanzania Hasheem Thabeet leo wameshiriki kwenye Kliniki ya mchezo huo kwenye viwanja vya Don Bosco jijini Dar es Salaam.
Mchezaji huyo yupo kwenye kampeni ya malaria, Nothing butNets.Net ambapo anashiriki kwa kugawa neti. Akiwa Don Bosco, mwenyeji wa mchezaji huyo na msafara wake alikuwa ni makamu Rais wa shirikisho la mpira wa kikapu nchini, TBF, Phares Magesa.
Kampeni ya Nothing butNets.Net ni kampeni inayohamasisha matumizi ya chandarua pamoja na kugawa kila nchi anayotembelea pamoja na kufundisha mpira wa kikapu.
Stephen aka Steph ni mchezaji wa timu ya Golden State Warriors akicheza nafasi ya guard ambapo kwenye msimu wa 2012–13 aliweka rekodi ya kufunga mitupo ya point tatu mingi zaidi.
Stephen akigawa Chandarua kwa wanafunzi wa Don Bosco
Stephen akisaini kitabu cha wageni Don Bosco, pembeni ni Makamu Rais wa shirikisho la mpira wa kikapu nchini, TBF, Phares Magesa
Stephen na Hasheem wakishow love na mashabiki
Stephen na Hasheem wakiingia uwanjani