Kama wewe si mtazamaji wa filamu za kibongo huenda sura ama jina la Skyner Ally ni geni kabisa. Au labda mara yako ya kwanza kumuona msichana huyu mrembo ni kwenye video ya Bob Junior ya wimbo wake Kimbiji.
Skyner Ally Seif ni kipaji kilichogunduliwa na Ray na tayari ameshaigiza kwenye filamu kadhaa zikiwemo ‘The Second Wife’, ‘What is It’, ‘Why I Did Love’, ‘I Hate My Birthday’, ‘Kizungumkuti’, ‘Unpredictable’ na sasa yupo location akiigiza kama mke wa Ray kwenye filamu mpya, Chicken Head.
Skyner kwenye set ya Chicken Head
Skyner ambaye aliolewa mwaka 2011 na aliyezaliwa mwaka 1992, ametokea kupata umaarufu kwenye fani hiyo na kwa muonekano wake Jacky Wolper na Irene Uwoya wakae chonjo.
Tazama Video aliyofanya kama queen ya Bob Junior - KIMBIJI
Tags:
From Bongo Movies