News Update: Mmoja wa wasichana wa Uingereza waliomwagiwa tindikali Zanzibar aruhusiwa kutoka hospitali




Mmoja wa mabinti wawili waliomwagiwa tindikali huko Zanzibar wiki iliyopita na baadae kurejeshwa nchini kwao Uingereza kwa matibabu ameruhusiwa kutoka hospitalini huku mwenzake akisubiri kufanyiwa upasuaji.


Kirstie Trup, (18) ambaye alimwagiwa tindikali na mwenzake Katie Gee, (18) ameruhusiwa kutoka katika hospitali ya ‘Chelsea and Westminster’ aliyopelekwa kwaajili ya matibabu, lakini anatikiwa kurudi tena hospitali alhamisi wiki hii kwaajili ya matibabu zaidi, ‘I can confirm that Kirstie has been temporarily discharged until Thursday when she’s back in for a skin graft. We won’t make any comments regarding Katie.’ Mama yake Kristie Mrs Trup, (49), aliliambia gazeti la ‘The Evening Standard’.


Msichana wa pili Gee ambaye anasemekana kuungua asilimia 80 ya mkono wake wa kulia na asilimia 50 sehemu nyingine ya mwili ameendelea kubaki hospitali akisubiri kufanyiwa upasuaji.


Wasichana hao ambao ni wanafunzi walikuja Zanzibar kama waalimu wa kujitolea ikiwa ni sehemu ya kujifunza, na wiki waliyokumbwa na tatizo la kumwagiwa tindikali ndio ilikuwa wiki yao ya mwisho kabla ya kurejea nchini kwao Uingereza.
Previous Post Next Post

Popular Items