Msanii wa Hip Hop, Nay Wa Mitego amesema haogopi vitisho anavyoendelea kupata baada ya watu aliowatuhumu kwenye wimbo wa mpya, Salam Zao’ kuwa walichukua pesa za rambirambi za msiba wa marehemu Albert Mangwair.
Kupitia akaunti zake za Facebook na Instagram, Nay ameanza kuandika na kufichua vitisho anavyopokea na huku akiwataka waliochukua pesa za marehemu Ngwair wazirudishe kimya kimya.
“Zipo nyingi zingine za vitisho,nitazipost zote watu wangu mujue leo nimeanza na iyo..!! Ukweli unauma sana!! siogopi vitisho vyenu,, pelekeni hela kwa ndugu wa marehem bado nafasi mnayo ata kimya kimya,, mi Nikifa sihitaji kamati za ki**enge kwenye msiba wangu, maana watu wanafanya misiba yetu mitaji yao,” ameandika Nay.