Mtoto wa Riyama ageuka kuwa kero kwa waongozaji wa filamu




Mtoto wa kike wa mwigizaji Riyama aliyejifungua hivi karibuni amegeuka kuwa kero wa waongozaji wa Filamu wa nchini kutokana na mwanadada huyo kwenda naye kwenye kila location anapotengeneza Filamu hivyo kusababisha usumbufu katika utengenezaji wa Filamu GPL wameripoti.
Akizungumza na gazeti la ijumaa mmoja wa waongozaji wa Filamu alisema kuwa mwanadada Riyama asipoangalia anaweza kupotea kisanii kwani kila unapotaka kumchezesha kwenye Filamu lazima umuandalie chumba cha kulala yeye na familia yake kutokana na mtoto wake mdogo huyo.
Habari inasema kuwa eti, mwanadada Riyama hawezi kwenda kulala mwenyewe na kumuacha bwana wake huyo, sasa baadhi ya wasanii wanamkwepa kitu ambacho kitamuathiri.
Naye Riyama Akizungumzia hilo alisema: “Kulala chumba kimoja na wasanii wenzangu ni kitu nisichokipenda. Ndiyo maana huwa napenda niwe na chumba changu mimi na baba mtoto wangu, mwanangu na dada wa kazi, kama mtu hataki basi siwezi kucheza filamu yake.”

Previous Post Next Post