Bohari ya Dawa Nchini (MSD), juzi ilikabidhiwa cheti cha ithibati cha Shirika la Kimataifa la Viwango (ISO) kutokana na kutoa huduma kwa ubora nchini.
Akikabidhi cheti hicho Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi aliipongeza MSD kwa kuingiakatika mchakato na hatimaye kupata cheti hicho.(P.T)
"Napenda kuchukua fursa hii kuipongeza kwa dhati Bohari Kuu ya Dawa, kwa kuingia katika mchakato huu na hatimaye kupata hati ya ithibati," alisema Dk Mwinyi.
Waziri huyo alisema kumekuwa na wimbi la uingizaji wa bidhaa duni zikiwemo dawa na kwamba nyingine zimeweza kupenya hata katika taasisi za Serikali na kuleta shida kwa wagonjwa wanaotegemea dawa.
Kaimu Mkurugenzi wa MSD, Cosmas Mwaifwani, alisema kutokana na cheti hicho sasa Watanzania watarajie huduma bora za dawa na vifaa tiba.
Alitaja mchakato wa kupata cheti hicho kuwa ni pamoja na kuandaa mpango wa ubora, malengo, viwango vya ubora.
"Tumefanya kazi na TBS na ndiyo wametushauri," alisema.
Tags:
Health