Kocha wa Chelsea Jose Mourinho ameiambia klabu ya Manchester United ikubali kumuuza Wayne Rooney kwa klabu yake ya Chelsea. (HM)
Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari, Mourinho alitoa mfano namna timu pinzani za Italia zinavyofanya biashara ya kuuziana wachezaji na akaishangaa Man United kukataa kumuuza Rooney kwa wapinzani wao na kuita ni mambo ya kizamani: "Hayo ni mambo ya kizamani ya kukataa kuuza mchezaji wako kwa timu ambayo mnacheza nayo ligi moja - hilo halisadii soko na pia wachezaji husika.
"Unaona nchini Italia, inavyotoke kila msimu bila matatizo yoyote. Mchezaji anaweza kutaka kuhama kutoka Milan kwenda Inter, kutoka inter kwenda Milan, kutoka Roma kwenda Juventus, kutoka Juventus kwenda Inter, na wanafanya hivi siku zote.
"Umeona Inzaghi, alicheza Juventus, Milan, Inter. Nadhani ni [Francesco] Totti pekee ambaye amekaa kwenye klabuy moja maisha yake yote. [Andrea] Pirlo – amecheza Inter, Milan, Juventus.
"Kwanini umuuze mchezaji kwenye ligi ya nje wakati unaweza kumuuza ndani ya ligi katika kuiimarisha zaidi ligi.
"Hivyo nadhani unapotaka kumuuza mchezaji na unalazimisha lazima auzwe nje ya nchi, nafikiri unakuwa hautoi mchango katika kuiimarisha ligi ya ndani ambayo timuyako inashiriki."
Pamoja na maneno haya ya Mourinho, David Moyes ameendelea kusema Rooney hauzwi, akisisitiza mshambuliaji huyo wa England bado ana jukumu kubwa ndani ya Old Trafford msimu huu.
Mourinho pia alithibitisha kwamba baada ya mchezo wa Jumatatu watatuma ofa nyingine ya mwisho kwa United: "Ngoja tuone tutakapotuma ofa nyingine kama watakataa tena, kwanini nini tutapoteza? Labda hiyo barua pepe.
"Majibu mawili ambayo tumepata kutoka kwa Manchester United yalikuwa 'hatukubaliani na ofa, hatuna mpango wa kumuuza mchezaji huyu'. Hayo ndio majibu rasmi waliyotupa."
Chanzo: shaffihdauda
Tags:
Sports