Mbali na DIamond Plutnumz: Wizkid wa Nigeria ni kati ya wasanii wa Afrika wanaotoza pesa nyingi kufanya show




Yawezekana Wizkid akawa hajapata jina kubwa sana kwa Tanzania kama ilivyo kwa wasanii wengine wa Bongo kama Diamond au ata wasanii wa Nigeria kama P- Square, J.Martins na wengine, lakini ni kati ya wasanii wa Afrika wanaolipwa pesa nyingi kwa show moja.





Wizkid ambaye anajulikana zaidi kupitia hit songs zake kama ‘Tease Me’ , hivi karibuni amefunguka kuhusu gharama anayotoza kwa show moja kuwa ni Naira M5 sawa na shilingi million 50, alifunguka alipokuwa anafanyiwa mahojiano na gazeti la Nigeria.

Kwa Tanzania kati ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya ambao kwa sasa wamethibitisha kutoza pesa nyingi kwa show moja ni staa Diamond Platnumz ambaye ameendelea kupata show za kitaifa na kimataifa kama mvua. Show ya Diamond aliyofanya Comoro mwezi June alilipwa million 38.

Nyimbo zingine zilizomtambulisha Wizkid aliyezaliwa mwaka (1990) ni pamoja na Don’t Dull, Love My Baby, Dance For Me na nyinginezo.




Previous Post Next Post