MAN UNITED NA CHELSEA ZATOKA SARE YA 0-0




ROONEY_aa5aa.jpg
Rooney akimdhibiti Ramires
KOCHA wa Manchester United, David Moyes amepeleka ujumbe kwa Chelsea kwamba Wayne Rooney hatahamia Stamford Bridge majira haya ya joto kufuatia mchezo wa usiku huu wa miamba hao uliomalizika kwa sare ya bila kufungana kwenye Uwanja wa Old Trafford.
Rooney alianza katika kikosi cha kwanza baada ya tetesi za muda mrefu majira haya ya joto kwamba atajiunga na Jose Mourinho Magharibi mwa London, lakini alipiga soka ya uhakika leo akiwa na uzi mwekundu.
Chelsea ilianza bila washambuliaji wake Fernando Torres na Romelu Lukaku walioanzia benchi, lakini gumzo zaidi ni kila upande kulalamikia kunyimwa penalti katika mechi hiyo.
Katika mchezo huo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Enlgand baina ya timu hizo, United ilianzisha washambuliaji watatu, Welebeck, Rooney na Van Persie. Dakika ya 65 Lampard alishika kabisa mpira kwenye eneo la hatari kufuatia shuti la Cleverley, lakini refa 'akapeta'.
Dakika ya 71 Ashely Cole alianguka kwenye eneo la hatari wakati akikabiliana na Jones na akalilia penalti na hata Mournho akaonekana kulalamika akiwa kwenye benchi.
Mchezo ulikuwa mkali na timu hizo zilishambuliana kwa zamu na baada ya mechi wachezaji walipongezana kwa mchezo mzuri.
Jose Mourinho alisema baada ya mechi mchezo ulikuwa wa haki na hadhani kama kuna iliyomzidi mwenzake uwezo, wakati Moyes alilalamikia penalti ya Lampard kuunawa mpira na kuwapongeza vijana wake kwa soka nzuri.
Kikosi cha Man United kilikuwa: De Gea, Jones, Ferdinand, Vidic, Evra, Valencia/Young dk67, Cleverley, Carrick, Welbeck/Giggs dk78, Rooney na Van Persie.
Chelsea: Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Cole, Ramires, Lampard, De Bruyne/Torres dk60, Oscar, Hazard/Azpilicueta dk93 na Schurrle.
ramiles_c1c0d.jpg
Amerudi kikosi cha kwanza: Rooney alianza katika kikosi cha kwanza na alicheza vizuri akipiga mashuti mazuri mawili yaliyokaribia kuzaa mabao Old Trafford
Previous Post Next Post