Mfanyabiashara maarufu mjini Moshi ambaye jina lake limehifadhiwa, anadaiwa kujirekodi video awakimlawiti mfanyakazi wake wa dukani. Video za mfanyabiashara huyo zinasemakana kusambazwa kupitia simu hasa kwa Whatsapp na sasa zinauzwa kwenye maduka ya Stendi Kuu ya Mabasi mjini humo.
Gazeti la Mwananchi limeandika:
Inadaiwa kuwa mfanyabiashara huyo kijana anayemiliki maduka matatu Stendi Kuu ya Mabasi, alirekodi video hizo kwa siri bila mfanyakazi wake huyo kujua na kuihifadhi kwenye kompyuta.
Haijajulikana ni nani aliyeingia katika kompyuta hiyo na kunakili picha hizo ambazo moja ina sekunde 45 na nyingine inayomuonyesha akimlawiti mfanyakazi wake huyo ikiwa na muda wa dakika nane.
Habari za uhakika zilizopatikana zimelidokeza gazeti hili kuwa kwa sasa mfanyabiashara huyo pamoja na mwanamke huyo wametoroka na hawajulikani walipo baada ya kubaini wanasakwa na polisi.
Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro, Robert Boaz alipoulizwa jana alisema ingawa hajaona video hizo, lakini kufanya mapenzi kinyume cha maumbile ni kosa la jinai hivyo watamtafuta mfanyabiashara huyo.
Kamanda Boaz alisema polisi wanamsaka ili ahojiwe kuhusiana na video na vitendo hivyo alivyoiita ni vichafu na kwamba kimsingi anatakiwa kujisalimisha mwenyewe ili kumaliza mambo.
News Via: Mwananchi
Tags:
Uncategolized