King and Prince of Pop: Collabo ya Justin Bieber na Michael Jackson yavuja mtandaoni (Audio)




Jana (August 16) wimbo wenye sauti za mtu na baba yake katika muziki Justin Bieber na marehemu Michael Jackson ‘Slave to the Rhythm’ umevuja mtandaoni.



Inawezekana umeshawahi kuusikia wimbo wenye jina hilo kutoka kwa Michael Jackson mwenyewe, wala hujakosea sababu original version ya wimbo huo iliyofanywa na Michael Jackson mwenyewe ilivuja mwaka (2010) mara baada ya kifo chake lakini haukupata umaarufu.

Katika remix ya ‘Slave to the Rhythm’ ambayo imesambaa jana mtandaoni, zinasikika sauti za Bieber lakini lakini pia sauti za MJ zimebaki na kufanya iwe ni remix ya mtu na baba yake au ‘King and prince of Pop’.

Ingawa bado haijawa wazi kama remix ya wimbo huo ilidhamiriwa kufanywa na kutoka kama collabo rasmi au laa, lakini kilichowazi ni kuwa Bieber huenda anajua nini kinachoendelea juu ya wimbo huo sababu baada ya remix hiyo kusambaa jana alianza kutweet kuhusu mfalme huyo wa Pop MJ;

“Excited for what is to come. MJ set the bar. Not only for music but for being an entertainer and how u treat the fans. Wish he was here…,” Justin alitweet na kuongeza. “All of it is not always easy but it is a blessing. We can change the world. I’m up for the challenge. Big things ahead! #greatness. love you.”

Isikilize hapo chini




Previous Post Next Post

Popular Items

WAKUU WA USALAMA KUHOJIWA KENYA