Ishara ya wingi wa mashabiki wanaohudhuria katika tamasha la muziki, pamoja na muitikio wa mashabiki pale msanii anapokuwa jukwaani akifanya mambo yake huwa ni majibu ya jinsi gani msanii husika amepokelewa na mashabiki hao.
Kwa kutumia vigezo hivyo msanii wa kike Brandy Norwood kutoka Marekani huenda ameondoka na tafsiri mbili, kuwa ameshuka kiwango au hana mashabiki Afrika Kusini baada ya kujikuta anatumbuiza mbele ya watu arobaini! ndio namaanisha 40 katika uwanja wa mpira unaochukua watu 90,000 huko Johannesburg, Afrika Kusini weekend iliyopita.
Brandy (34) ambaye alipangwa kutumbuiza katika siku ya michezo na utamaduni ya Mandela ‘Nelson Mandela Sport and Culture Day’ Jumamosi iliyopita (August 17), alilazimika kukatisha show baada ya kuimba hit songs zake mbili kama ilivyoripotiwa na mitandao mbalimbali. Kibaya zaidi show hiyo iliyokuwa inarushwa na kituo cha televisheni cha nchi hiyo matangazo yalikatishwa kuoneshwa pia.
Inasemekana onesho la mwimbaji huyo wa “Boy Is Mine” halikuwa limetangazwa vya kutosha hivyo kusababisha maelfu ya watu waliokuwa wamejaa uwanjani hapo mapema katika matukio yaliyotangulia katika sherehe hizo siku hiyo, kutofahamu uwepo wa Brandy na kuamua kuondoka karibu wote mpaka kubaki wasiozidi 40 usiku wakati ambapo Brandy ndio alipaswa kuanza onesho lake.
Matukuo yaliyotangulia mchana kabla ya onesho la Brandy ni pamoja mpira wa soka, rugby pamoja na performance kutoka kwa wanamuziki mbalimbali wakiwemo Salif Keita , D’Banj na wengine, na Brandy ndiye alipangwa kufunga show usiku huo.
Tukio la watu kubaki wachache sana wakati Brandy anapanda jukwaani lilifichuliwa na msanii wa Afrika Kusini aitwaye Kabomo aliyekuwa uwanjanai hapo na kutweet kile alichokiona akiwa mmoja wa watu 40 waliobaki kushuhudia onesho la mkongwe huyo wa R&B.
“I have no words for what I just witnessed…,Brandy [just] performed to an empty stadium. With the stadium lights on. It was late. People didn’t know there was a concert after the games. No one knew Brandy was around,”Alitweet.
“I have no words for what I just witnessed…,Brandy [just] performed to an empty stadium. With the stadium lights on. It was late. People didn’t know there was a concert after the games. No one knew Brandy was around,”Alitweet.
Brandy na wandaaji hawajazungumza chochote kuhusu tukio hilo.