BENZEMA ANAYEWATOA UDENDA ARSENAL AENDELEA KUNG'ARA REAL



benzema 15e9d
Karim Benzema akifumua shuti kumfunga kipa wa Granada, Roberto Fernandez (HM)
benzema2 ed919
Karim Benzema akipongezwa na Cristiano Ronaldo baada ya kufunga bao lake la pili la msimu
MSHAMBULIAJI anayetakiwa na Arsenal, Karim Benzema ameiongoza timu yake kushinda mechi ya pili ya La Liga baada ya usiku huu kufunga bao pekee katika ushindi wa Real Madrid wa 1-0 dhidi ya Granada.
Mfaransa huyo alimtungua kipa wa wenyeji, Roberto Fernandez dakika ya 10, baada ya kupata pasi ya Cristiano Ronaldo akiwa kwenye boksi.
Wakati huo huo, kipa Iker Casillas, nyota mwingine wa Madrid anayetakiwa na kocha wa Gunners, Arsene Wenger, ameendelea kusota benchi.
Kikosi cha Real Madrid kilikuwa: Diego López; Arbeloa, Sergio Ramos, Pepe, Marcelo/Nacho, Modric, Ozil/Casemiro, Di María/Carvajal, Isco, Ronaldo na Benzema.
Granada: Roberto; Nyom, Diakhaté, Mainz, Angulo; Iturra, Yebda/Fran Rico, Brahimi, Benítez/Buonanotte, Piti na El Arabi/Riki. 
Previous Post Next Post