Mnyama TID a.k.a too much info in town amepata shavu la kwenda kupiga show mjini Muscat katika sikukuu ya Eid el Fitri mwanzoni mwa mwezi ujao.
Akionesha furaha yake baada ya kupata mchongo huo, TID ameshare picha baada ya kusaini mkataba wa show.
“For the first time in bongo flava history T.I.D and TopBand to perfom in muscat on Eid el Fitri as am signing the contract with president Suleiman….haya wanaona gere,” ameandika.
Wakati huo huo, TID anatarajia kuachia ngoma mpya hivi karibuni iitwayo ‘Gere’ ambayo amemshirikisha mwanadada Maunda Zorro.