Ushindani wa biashara ya smart phone unazidi kukuwa na kufanya kila kukicha makampuni pinzani kama Samsung na Apple kuja na matoleo mapya ya bidhaa zao zinazoleta ushindani mkubwa wa soko. Kampuni ya Samsung imepeleka sokoni toleo jipya la Galaxy S4 Active isiyongia maji wala vumbi ‘waterproof and dustproof version’.
Kampuni ya Samsung yenye makao yake makuu Korea kusini imesema imetengeneza toleo hili la Galaxy S4 Active isiyopitisha maji wala vumbi, ikiwalenga wazazi kwa kuwasaidia kuepusha ajali na uharibifu unaoweza kusababishwa na watoto.
“We know a lot of parents use their phones to show children content. We ended up going to a lot of family homes where we were shown a graveyard of smashed phones”. Alisema Luke Mansfield mkuu wa ‘ Samsung’s Europe innovation team’ alipozungumza na The Times.
Simu hiyo inauwezo wa kukaa ndani ya maji kwa dakika 30 na kupiga picha majini kwa kutumia ‘waterproof camera’.
Simu ya Galaxy S4 Active ambayo ilitambulishwa (May) imeingia sokoni mwezi huu (July) na inagharimu £480 sawa na karibia million 1 na laki 2.