Picha: Jina la Diamond Platnumz Laandikwa kwenye matatuu ya kenya...



Matatu a.k.a ‘mathree’ moja ya nchini Kenya imeonekana ikiwa imejaa chata zenye majina ya msafi Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platnumz kitu ambacho kinaweza kufanya uhisi anaubia.
Ofcourse nina uhakika Platnumz anaubia tena mkubwa sana na wahusika wa matatu hiyo, sababu wenye matatu hiyo wanaonekana kuwa mashabiki wake wakubwa ukizingatia Diamond anaubia na mashabiki wake wote.(bila mashabiki msanii si kitu)
matatu
Hivyo ndivyo hit maker wa ‘Kesho’ anavyopendwa nchini Kenya, kama picha inavyojieleza matatu hiyo kwa mbele imeandikwa ‘Wasafi, Diamond’, ubavuni imeandikwa ‘Wasafi’, na nyuma ya gari imepigwa chata inayosomeka ‘Platnum, zzacha wasafi’.
Sina uhakika kama wakenya hao wanajua huyo zacha waliyemuandika ni producer, kuna uwezekano wametoa katika moja ya nyimbo za Diamond ambazo amehusika kuproduce.
Picha hiyo iliyowekwa katika akaunti ya Wasaficlassic Instagram ilisindikizwa na caption “This is what we called TRUE LOVE… #Kenya Mme tisha saana #WCB for ever baby #Cocaboys “.
Platnumz anategemewa kufanya show kubwa mbili nchini Kenya mwezi ujao (August) ikiwa ni sehemu ya list ndefu ya show alizofanya na anazotegemea kuzifanya sehemu tofauti ndani na nje ya Tanzana kabla mwaka huu haujaisha.
Previous Post Next Post

Popular Items