Big Brother Africa “The Chase” Waandika Haya kuhusu DJ PQ.




Dj kutoka Clouds Media Group ndiyo atakuwa Dj wa kwanza kuwarusha washiriki wa Big Brother waliochanganyika kutoka Ruby na Diamond. Mtandao official wa Big brother Africa the Chase ambayo unaiona pekee kupitia Dstv, wameendelea kuandika kwamba Dj PQ jina lake la u-dj linatokana na jina lake la kwanza Peter na Q ni quick kutokana na kasi yake anapokuwa kazini.

Usikose kuona jinsi Dj PQ anavyoingia kwenye list ya madj waliowarusha washiriki wa Big brother tangu ianze season ya mwaka huu. Dj PQ ambaye alianza kupata fans wengi mwaka 1998 baada ya kushinda Dj competition na kupewa crown ya Smart Boy Dj, leo usiku mida ya saa tano kwa saa za Tanzania atakuwa anawarusha washiriki wa Big brother.
Previous Post Next Post