Sheria mpya inayozuia uvaaji suruali chini ya makalio (Kata K) yawakasirisha ma-rapper wa Marekani


Sheria mpya ya kuzuia uvaaji wa suruali chini ya makalio maarufu kama ‘Kata K’ au ‘mlegezo’ imewakera ma rapper mbalimbali wa Marekani ambao wengi wao wameitafsiri kama kitendo cha kibaguzi ambacho serikali ya jiji la Wildwood imeamua kufanya.
Sheria hiyo inawataka watu wote wanaoingia katika jiji la Wildwood, New Jersey, Marekani kuhakikisha suruali zao hazishuki zaidi ya inchi 3 chini ya kiuno cha mvaaji, atakaekiuka sheria hiyo kwa mara ya kwanza atawajibika kulipa faini ya dola 25 hadi dola 100, na atakayekiuka mara ya pili na kuendelea atatozwa faini ya mpaka $200. Adhabu nyingine inayoweza kutolewa ni pamoja na kufanya kazi za jamii kwa saa 40.
Mmoja wa ma rapper waliokerwa na sheria hiyo mpya iliyopitishwa na jiji la Wildwood huko New Jersey Marekani ni The Game. Akiongea na mtandao wa TMZ Game ameonekana kuchukizwa na sheria hiyo na kusema kuwa hawawezi kuwapangia watu jinsi ya kuvaa nguo na kuongeza kuwa hizi sio enzi za utumwa. “They trying to get people to not sag, please. Can’t tell people how to wear their f***ing clothes. What time are we in? This ain’t the f***ing slave days. F*** that.”
Game aliongeza kuwa yeye ataendelea kuvaa mlegezo na watu watano wa kwanza kukamatwa kwa kosa hilo atawalipia faini yeye na ataenda huko huku akiwa amevaa kata K, “I am with the sagging movement. First five people to get fines, I will pay their tickets … I will go there and sag cause I am a sagging Sagittarius.”
Rapper mwingine kutoka kundi la Bone Thugs-n-Harmony aitwaye Bizzy Bone aliuliza kama sheria hiyo inawalenga watu weusi na kusema huo ni ubaguzi na ujinga “Are they talking about black people? How can they do that? This is racist and ridiculous.”
Rapper mwingine aliyeonekana kutokubaliana na sheria hiyo ni Mac Miller ambaye hajatofautiana na Game na Bone kwa kusema huo ni ujinga na kuongeza kuwa yeye ataendelea kuvaa mlegezo popote aendapo, “I just think that’s ridiculous because no one has time to do that much community service. I sag and will sag anywhere I go.”
Sheria hiyo inategemewa kuanza kufanya kazi mwezi ujao (June) katika jiji la Wildwood, New Jersey nchini Marekani.
Previous Post Next Post